Fid Q Avunja Kimya Chake Kuhusu Safari Yake Ya Mziki, Amshukuru Prof Jay.
“ Asante @professorjaytz kwa kunirudisha njiani.. ni ukweli YATAKA MOYO.. sanaa ya BONGO nzito/ washkaji wamegeuka NYOKA kama ile ( ya MUSSA ) FIMBO “ 📌
Kihistoria:
Nilikua ninaelekea kuchana DAFTARI langu la MISTARI ( RHYME BOOK ) na kuachana na masuala ya sanaa na miziki kwa ujumla.. lakini maamuzi hayo yalisitishwa ghafla baada ya kumsikia mmoja kati wakali ambao nishawahi kuzishuhudia HUSTLE zake kabla hajafanikiwa kisanaa.. akinikumbuka kwa kunitaja jina langu ( katikati ya majina ya WAKALI wengi wa kipindi hicho ) kwenye ngoma yake na kunisisitiza ya kwamba nifanye MAVITU kwani wakati ndio huo. Sikuwa na ngoma yoyote wala kuwahi kuingia studio kipindi hiko.. Prof alinijua kwa kupitia SHOWS tu.. Mimi ndio yule aliyekua anawakilisha Mwanza kwenye show yoyote yenye msanii mkubwa na ilikua ni lazima niondoke na kijiji.
Kwa ufupi: safari yangu ya kuingia studio kurekodi ilichagizwa sana na hiki kibao cha Prof na ninafikiri ilikua hivyo kwasababu ya kufahamiana nae tangu enzi zile akiwa ni mwanafunzi,na Mwanza alikua anakuja likizo kumtembelea Maza ake ambaye alikua anafanya kazi posta, ilinipa faraja na hamasa ya hali ya juu kumuona mmoja kati ya wale ambao tushawahi kukutana na ku-vibe akifanikiwa kwenye game na na pia nilivutiwa sana na kitendo cha yeye kunikumbuka kwenye ufalme wake kiasi cha kutaja jina langu kwenye MEZA ya FURSA.. ( well, hivyo ndivyo nilijisikia baada kusikia amenitaja)
Nimalize kwa kusema A small gift will do if your heart is big enough .
Hapo Jana JUMAPILI professor jay atazindua rasmi mfuko wa kuchangia wagonjwa wa FIGO ..