Arsenal Kumkosa Havertz Msimu Mzima

Share this story

Arsenal itamkosa mshambuliaji wake Kai Havertz katika mechi zote zilizobakia msimu huu baada ya kupata maumivu ya misuli katika kambi ya timu hiyo inayoendelea Dubai.

Hiyo ni habari mbaya kwa Arsenal katika kipindi ambacho inawakosa nyota wengine watatu wa ushambuliaji, Bukayo Saka, Gabriel Jesus na Gabriel Martinelli kutokana na majeraha.

Bukayo Saka atarejea uwanjani hivi karibuni kama ilivyo kwa Martinelli lakini Jesus atakuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima ambapo sasa ataungana na Havertz ambaye ndio amekuwa tegemeo la Arsenal msimu huu.

Kumkosa Havertz ni pigo kubwa kwa meneja wa Arsenal Mikel Arteta kwani Mjerumani huyo ndiye amekuwa akitumika kuziba pengo la kukosekana kwa mshambuliaji wa kati hivyo maumivu yake hapana shaka yanaweka shakani ndoto ya timu hiyo kutwaa mataji msimu huu.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Major Setback for Raila as 16 Countries Given New Directive
Next post Law Society of Kenya President Faith Odhiambo Wins Commonwealth Law Conference Rule of Law Award