
Aliyependekeza Jina La Tanzania Aaga Dunia
Mohamed Iqbal Dar, aliyependekeza jina la Tanzania katika shindano la kutafuta jina la taifa mwaka 1964, ameaga dunia akiwa usingizini jijini Birmingham, Uingereza, alikokuwa akiishi.
Iqbal alikuwa mmoja wa wanafunzi 80 waliopendekeza majina, na pendekezo lake likachaguliwa kuwa jina rasmi la taifa baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 18 na alipokea zawadi ya shilingi 200 za wakati huo kama mshindi wa shindano hilo.
Tanzania imempoteza mtu aliyekuwa sehemu ya historia yake muhimu