Vilabu vya Norway vyapiga kura kufuta VAR
Taarifa kutoka nchini Norway inaeleza kuwa Vilabu vimepiga kura ya kutaka kuiondoa teknolojia ya VAR kutumika katika ligi yao kwa sababu Ina unyonyaji mwingi ndani yake kwa baadhi ya a vilabu.
Kwa kuwa kura nyingi zimedai VAR iondolewe hakuna namna itaendelea kuwepo tena hivyo Ligi hiyo itarudi kuchezwa bila VAR
Matokeo ya kura yalipelekea pendekezo kwamba Shirikisho la Soka la Norway, NFF, lipige muhuri matokeo. NFF inatarajiwa kufanya uamuzi wa mwisho mwezi Machi, ingawa ESPN inaripoti kwamba baraza linaloongoza bado linaweza kubatilisha upigaji kura. VAR ilianzishwa kwenye Eliteserien mwaka wa 2023. Lakini mashabiki kote nchini wamekashifu zaidi matumizi ya mfumo huo. Mchezo wa Rosenborg dhidi ya Lillestrøm uliahirishwa mapema msimu huu, kwa sababu wafuasi walirusha keki za samaki uwanjani wakipinga VAR.