Marvel iko tayari kumtangaza tena T’Challa kama Black Panther.
Kampuni ya filamu ya Marvel Studios inapanga kumtambulisha tena T’Challa kama Black Panther kupitia filamu zijazo ikiwa ni pamoja na Avengers: Doomsday na Secret Wars.
Wadadisi wa mambo wanafichua kuwa, Uamuzi huu unakuja miaka minne baada ya kifo cha Mwigizaji Chadwick Boseman, na mwigizaji mpya anayetarajiwa ataigiza kama mhusika mkuu huku akiheshimu urithi wa Boseman.
Baada ya Shuri kuchukua vazi la Black Panther katika Black Panther: Wakanda Forever, hadithi ya Marvel inatarajiwa kupanuliwa na kufungua njia ya kurudi kwa T’Challa. Ripoti zinaonyesha kuwa kampuni hiyo inafanya kazi kwa karibu na familia ya Boseman ili kuhakikisha mabadiliko hayo ni ya heshima. Avengers: Doomsday imepangwa kutolewa mnamo Mei 1, 2026.