Kipa Emiliano Martinez Ashinda Tena Golikipa Bora wa Dunia

Share this story

Golikipa wa klabu ya Aston Villa raia wa Argentina, Emiliano Martinez (32) ameshinda tena tuzo ya Golikipa bora wa Dunia katika sherehe za ugawaji wa tuzo hizo nchini Ufaransa.

Martinez ambaye amekuwa sehemu ya kikosi cha Aston Villa kilichomaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza 2023/24 pamoja na golikipa tegemezi wa Argentina katika kikosi kilichoshinda michuano ya Copa America 2024 ameshinda tuzo hiyo inayojulikana kama ‘Yashin Trophy’ kwa mara ya pili mfululizo baada ya kushinda kwa mara ya kwanza mwaka 2023.

Martinez ameshinda tuzo hiyo kwa kuwashinda wapinzani wake kama Unai Simón (27) anaedakia klabu ya Athletic Bilbao ya Uhispania na Timu ya Taifa ya Hispania ambapo aliisaida timu yale kushinda ubingwa wa michuano ya UEFA Euro, pia Martinez amembwaga golikipa wa Dortmund na Timu ya Taifa ya Uswizi, Gregor Kobel (26) ambaye alifanya vizuri na klabu yake licha ya kupoteza katika mchezo wa fainali la Ligi ya Mabigwa dhidi ya Real Madrid.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post RODRI WINS THE BALLON D’OR 2024!
Next post Lamine Yamal Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi.