Idris Elba Afunguka Tena Nia Yake ya Kuja Kuishi Afrika
Mwigizaji nyota wa Filamu, Idris Elba amesema anatarajia kuhamia Afrika katika kipindi cha Miaka 10 ijayo na huenda akaishi katika maeneo ya Zanzibar, Accra nchini Ghana au Freetown huko Sierra Leone na lengo kukuza tasnia ya Filamu
Elba ambaye Januari 2023 alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu huko Davos, Switzerland amesema “Kwa hakika nafikiria kutulia hapa, katika Miaka mitano ijayo, 10, Mungu akipenda. Niko hapa ili kuimarisha tasnia ya filamu. Huo ni mchakato wa Miaka 10 sitaweza kufanya hivyo kutoka ng’ambo, nahitaji kuwa ndani ya Bara.”
Aidha, amesema lengo ni kubadili mtazamo kuhusu Afrika inavyochukuliwa ikiwemo kuwa ni sehemu ya Vita, Ukoloni, Umasikini tofauti na uhalisia huo ambao umesambazwa kwenye baadhi ya Filamu na machapisho