David Beckham : Sababu Za Kumchagua Messi Badaya Ya Cristiano
“Ilikuwa inawezekana kumsajili Cristiano Ronaldo na kumpa nguvu kama ambayo Lionel Messi anayo huku Marekani,
Lakini nilimchagua Lionel Messi kwa sababu ni moja ya wachezaji walioifanya hadhi ya soka la bara la America kuwa na hadhi”
“Ninamheshimu sana Cristiano Ronaldo kwa kuwa ni mchezaji mkubwa lakini nimemchagua mtu mwenye historia na mpira wa miguu.
Nilimfuata kwenye klabu ya PSG ili kumshawishi kutoendelea na klabu hiyo pindi mkataba wake utakapokuwa umemalizika.
Lakini pia aliniambia chaguo lake kubwa ilikuwa ni kurudi FC Barcelona kwa kuwa ndiko nyumbani kwake haswa
Ila Nashukuru nimefanikiwa kumpata ndani ya Inter Miami”