Aaron Wan-Bissaka ajiunga na West Ham

Share this story

West Ham wamemsajili mlinzi wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka kwa kitita cha pesa £15 milioni kwa mkataba wa miaka saba.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 26 ni mchezaji wa nane kusajiliwa na West Ham katika dirisha hili la uhamisho. Wachezaji hao saba ni Jean-Clair Todibo, Crysencio Summerville, Luis Guilherme, Niclas Fullkrug, Wes Foderingham, Max Kilman na Guido Rodriguez.

Wan-Bissaka alionyesha furaha yake kujiunga na Wananyundo hao.

Wan-Bissaka alijiunga na Manchester United mnamo Juni 29, 2019 kwa mkataba wa miaka mitano kutoka Crystal Palace kwa kitita cha pesa £50 milioni. Alifanikiwa kufunga mabao mawili kwa mechi 190 alizoshiriki.

Alikuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer wakati wake hadi akaondoka mwaka wa 2021.

Hata hivyo, kocha Eric Ten Hag alipofika Wan-Bissaka akapoteza muda wa kucheza. Hadi kuondoka kwake alicheza mechi 64.

Mashetani Wekundu wanaripotiwa kumtaka beki wa pembeni wa Bayern Munich, Noussair Mazraoui kama mbadala wake, mchezaji ambaye West Ham pia walikuwa wameonyesha nia ya kutaka kumnunua.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Shakib Cham breaks silence on marital issues with Zari Hassan: ‘No marriage can last without respect’
Next post Beatrice Chebet Promoted to Police Corporal After Double Olympic Triumph