Serem, Kibiwot na Koech wafuzu fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji

Share this story

Amos Serem, Abraham Kibiwot na Simon Koech wamefuzu fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwenye Olimpiki ya Paris 2024 Jumatatu usiku.

Serem nusura akose kufuzu baada ya kusukumwa akiruka kizuizi cha mwisho lakini akarudi nyuma na kuruka. Aliwafuata aliokuwa nao wakiongoza na kumaliza wa sita katika mchujo wa kwanza.

Hata hivyo, aliwasilisha malalamishi na kupewa nafasi ya kufuzu. Alitumia muda wa dakika 8:18.41. Aliyeshinda mchujo huo ni Soufiane El Bakkali (8:17.90) wa Morocco. Wa pili alikuwa Leonard Chemutai (8:18.19) wa Uganda. Aliyekamilisha tatu bora ni Getnet Wale (8:18.25) wa Uhabeshi.

Kibiwot alimaliza wa tatu katika mchujo wa pili akitumia dakika 8:12.02. Mohamed Tindouft (8:10.62) wa Morocco alishinda. Wa pili alikuwa Samuel Firewu (8:11.61) wa Uhabeshi.

Simon Koech (8:24.95) aliibuka wa tatu. Aliyechukua nambari ya kwanza alikuwa Lamecha Girma (8:23.89) wa Uhabeshi. Kenneth Rooks wa Marekani alimaliza wa pili kwa dakika 8:24.95. 


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Noah Lyles ndiye bingwa mpya kwenye mita 100
Next post Political parties registrar Nderitu confirms Omar as UDA Secretary General