Arsenal Yapokea Kichapo Cha Liverpool, Yatingwa mabao 2-0
Timu ya Arsenal ilipokea kichapo kutoka kwa timu ya Liverpool baada ya kupigwa mabao mawili kwa sufuri kwenye Ligi ya Soka ya kuwania kombe la Carabao. Kitumbua cha Arsenal kilianza kuingia mchanga dakika ya 19 pale Diogo Jota alipoweka nyavuni bao la kwanza. Mchezaji huyo aliwehakikishia Liverpool ushindi dakika ya 77″ baada ya kufunga bao la pili na kuzika matumaini ya Arsenal kuingia fainali.
Bao la pili kutoka kwa Diogo Jota liliwapeleka Wekundu hao kwa ushindi wa 2-0 na kukata miadi na Chelsea uwanjani Wembley katika fainali ya Kombe la EFL.