“Raundi Hii Siongei Na Mtu” Viongozi Wa ODM Wa Pwani Wamwidhinisha Joho Kuwa Rais 2027
Aliyekuwa Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amesema hatamsikiliza yeyote anayemshauri kusitiza azma yake ya urais. Joho alisema kuna wanachama wenzake wa chama cha ODM ambao wamekuwa wakimshauri kuenda pole pole katika mipango yake ya kujaribu kuwania uraisi kwa mara ya kwanza.
“Kuna watu katika ODM, ambao wananipigia simu wakisema naenda kasi na kwamba niende kwa mazungumzo. Sizungumzi na mtu yeyote, tutazungumza kwenye sanduku la kura likifika,” gavana huyo wa zamani alisema.
Gavana huyo wa zamani alisema hatatazama nyuma kwani anatumai kumrithi Raila ikiwa atapata wadhifa wa AU kufikia 2026.
Joho alithibitisha kwamba ameanza ombi lake la Ikulu na hatalegea. “Mimi ndo nimeanza na sirudi nyuma. Sirudi nyuma. Na wakati huu, watajua hadi wapwani watahesabiwa katika Kenya hii.”
Viongozi wa Pwani walioteuliwa na chama cha Orange Democratic Movement (ODM) wamemuidhinisha aliyekuwa Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho kugombea kiti cha urais 2027. Viongozi hao walisema ni wakati mwafaka wa Pwani kuwa kwa kinyang’anyiro cha kuwa rais ili kuwa rais wa sita wa Jamhuri ya
Joho alizungumza Jumamosi mjini Malindi, kaunti ya Kilifi, akiwa na uongozi wa pwani walipokutana kuadhimisha siku ya 12 ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Aliwataja watu wa Kaunti ya Kilifi kuwa wafuasi wakubwa wa umoja wa pwani.
Joho alisema yeye ndiye anayestahili zaidi kuwa mrithi wa Raila Odinga.
Waliohudhuria ni pamoja na mwenyeji na mbunge mashuhuri wa Malindi Amina Mnyazi, Seneta wa Kilifi Stwart Madzayo, Seneta wa Kwale Boy Juma Boy, Seneta wa Mombasa Mohamed Faki, Mwakilishi wa Kike wa Kilifi Getrude Mbeyu, Mwakilishi wa Wanawake wa Mombasa Zamzam Mohamed Mbunge Mishi Mboko, Mbunge wa Kisauni Rashid Benzimba, Mbunge wa Magarini Harrison. Kombe, Mwakilishi wa Wanawake wa Mombasa Zamzam Mohamed, na Mbunge wa Mvita Machele Mohamed.