Wanajeshi wa China wasema ‘wamejiandaa kwa vita’ katika zoezi kubwa la kijeshi

Share this story

Wakati dunia ikiwa bize na vita huko Ukraine na mashariki ya kati, Taiwan na China nao wanaendelea kutunishiana misuli vikali ambapo mapema mwezi huu China imefanya zoezi kubwa la kijeshi kukizunguka kisiwa hicho inachoamini ni eneo lake. Mazoezi hayo yamefuata baada ya siku chache kwenye maadhimisho ya uhuru wa Taiwan ambapo rais wa Taiwan Dr. Lai Ching-Te aliapa kwamba Taiwan ni taifa huru la kidemokrasia na kamwe sio sehemu ya China na kamwe halitakubali kutwaliwa na China hata kijeshi.

Taiwan ni kisiwa kikubwa chenye utajiri wa teknolojia hususan ya vitunza kumbukumbu maarufu kama micro chips duniani, ikiwa na kampuni kubwa zaidi la bidhaa hizo la TSMC

Marekani ndio taifa rafiki mkuu wa Taiwan na ndio inayowauzia silaha Taiwan. Pia Marekani ilishatoa tamko rasmi kwamba itailinda Taiwan hata kijeshi itakaposhambuliwa na China. Kauli hiyo ilitolewa na Rais Joe Biden Septemba mwaka 2022 kama ilivyoripotiwa na shirika la habari duniani Reuters (taarifa hiyo nmekuekea hapo chini kwenye comments).

Biden alipoulizwa atailinda kwa misaada tu ya silaha kama Ukraine au hata askari watapigana akasema NDIO.

Hii ina maana China ikithubutu kuivamia Taiwan inaingia kwenye vita moja kwa moja na Marekani. Ikumbukwe pia kuwa Marekani, Taiwan na Ufilipino zinafanyaga mazoezi ya pamoja ya kijeshi kila mwaka

Kitisho kikubwa walichonacho China katika mvutano huu ni uchumi wake ulioimarika mno, miundombinu yake mikubwa ya kiuchumi ikiwemo bwawa kubwa la umeme na umwagiliaji maarufu kama Gorges Dam n.k

Inasemekana Marekani imeiuzia Taiwan silaha nyingi mno za kisasa za kivita (sophisticated weapons). Pia Taiwan ni kati ya visiwa vyenye teknolojia ya hali ya juu kuzidi mataifa mengi duniani hivyo uwezo wao katika medani sio mdogo hata kidogo


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post CJ Martha Koome Appoints 3 Judges to Hear Gachagua Petition Against Impeachment
Next post Thomas Tuchel is in talks to become the next England manager