
TANZANI: ATCL, TTCL zapata hasara ya mabilioni.
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limepata hasara ya shilingi bilioni 91.8 za Tanzania, ikiwa ni ongezeko la asilimia 62 kutoka shilingi bilioni 56.6 mwaka uliopita ambapo hasara hiyo imetokana na gharama kubwa za matengenezo ya ndege na hitilafu za injini ambapo ndege aina ya Airbus zilikaa muda mrefu zikisubiri injini.
Haya yamebainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ambaye pia amesema kampuni hiyo ilitumia kiasi cha shilingi Bilioni 99.8 kama ruzuku kutoka serikalini na kama wasingepata ruzuku hii hasara halisi Ingekuwa Bilioni Tsh.191.6.