Takriban watu 6 wamefariki katika mkanyagano jioni ya leo nje ya uwanja wa mchezo kati ya Cameroon na Comoros.
Takriban watu 6 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kukanyagana nje ya uwanja wakati wa mechi kati ya Cameroon na Comoro kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon.
Kanda za video zilionyesha mashabiki wa soka wakihangaika kupata njia ya kuingia uwanja wa Paul Biya katika kitongoji cha mji mkuu Yaounde. Maafisa wa mechi walinukuliwa wakisema kwamba watu 50,000 hivi walikuwa wakijaribu kuhudhuria ila masharti yalikuwa yamewekwa kudhibiti usambazaji wa virusi vya korona.