Mwanasiasa Mkongwe Chirau Ali Mwakwere azindua kampeni za kumrithi Gavana Salim Mvurya
Mwanasiasa Mkongwe Ali Cherau Mwakwere azindua kampeni za kumrithi Gavana Salim Mvurya. Mwanasiasa huy aliwahi jaribu kugombea kiti hicho mwaka wa 2017 na kushindwa na gavana wa sasa Salim Mvurya.
Kwenye uzinduzi huo uliofanyika mjini Vanga, Mwakee aliahidi kinyang’anyiro kikali mwaka huu wa uchaguzi. Mwakwere mwenye amewahi hudumu kama waziri wa serikali kuu kwa mda mrefu alisema bado ako na nguvu ya kisiasa eneo hil la kwale na alikuwa anawaonea huruma wenye wanamdharau kwa sababu watashtuka wakati wa uchaguzi.
Mnano mwaka wa 2013, mwanasiasa huyo alipoteza kiti cha usenata kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi baada ya kushindwa na marehemu Boy Juma.
Kwenye ratiba yake ya kufikia wananchi wa Kwale kutafuta kura, anatarajiwa kutembelea wadi zote 20.
Mwakere aliahidi kupigana na wafisadi kwa kaunti ya Kwale, waliofuja pesa ya umma. Vile vile aliahidi kupigana na umaskini eneo hilo na kutengeneza nafasi za ajira kwa vijana.
Mwanasiasa huyo pia aliahidi kuinua maisha ya familia za wakaazi wa kwale kwa kuwaletea vitega uchumi na kuhakikisha kila familia iko na mapato dhabiti. Pia aliahidi kukuza elimu kupitia mpango wa udhamini wa bursary.
Mbunge huyo wa zamani wa Matuga pia aliahidi kukuza uhusiano wa county ya Kwale na serikali kuu.
Mwana siasa huyo anatarajiwa kugombea kiti hizo kupitia tiketi ya chama cha Wiper