
Mwanamuziki nguli wa Kenya Ally B amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Mwanamuziki Kutoka Pwani, Ally B Khamis anayefahamika kwa vibao vyake Maria & Bembea amefariki dunia katika hospitali ya Coast General.
Ally B alikuwa mmoja wa mastaa wakubwa kutoka ukanda wa Pwani. Muziki wake Kadzo, Maria, na Bembea miongoni mwa wengine utahifadhi kumbukumbu za nguli huyo .

Mwanamuziki huyo anayeishi Pwani aliaga dunia Jumatano, Novemba 1. Ally B ambaye hivi karibuni alikuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu na kuruhusiwa kutoka hospitalini, alikumbwa na matatizo alipokuwa akielekea hospitalini.