MWANAJESHI WA KDF ALIYEFARIKI BAADA YA GARI LAO KUKANYAGA KILIPUZI GARISA AZIKWA NYUMBANI KWAKE MWATATE
Mwili wa mwanajeshi wa KDF aliyefariki baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi eneo la Garissa amezikwa nyumbani kwake Mwatate kaunti ya TaitaTaveta.
Mkasa huo uliotokea tarehe 6 juni 2022 ulihusisha mwendazake Hillary Mwaita na alilazimika kuendelea na matibabu baada ya matibabu.
Jumatatu Tarehe 13 mwezi huu alifanyiwa upasuaji ambao ulienda vizuri na hali yake ilidorora tarehe 15 na mwishowe akaaga dunia.
Mwenda zake alijiunga na kikosi cha jeshi mwezi wa octoba mwaka wa 2010.
Hillary Mwaita mwenye umri wa miaka 32 amemuacha mjane, Dorah Wawuda na watoto watatu.