Mombasa kuendelea kutoza ada ya Sh700 ya kuegesha lori za biashara
Mahakama kuu ya Mombasa imekataa kutoa maagizo ya muda ya kusitisha uamuzi wa serikali ya kaunti ya Mombasa kuongeza ada ya kuegesha magari makubwa na ya kibiashara hadi Sh700. Jaji Olga Sewe alisema maagizo yaliyoombwa na Chama cha Wasafirishaji Barabara nchini Kenya yatalingana na kusimamisha wosia wa kisheria na masuala ya serikali ya kaunti.