MH. BWIRE : Twiga Foods Wanaleta Ushindani Kwa Wakulima Wadogo Taveta
Mbunge wa Taveta Wakili John Bwire siku ya Jumatano, tarehe 19 Oct, aliweza kufanya mkutano wa ushirikiano na Twiga Foods, KWS, AFC, Serikali ya Kaunti, na Taasisi ya Micro-Enterprise Support Programme Trust kuhusu jinsi ya kuwawezesha na kuwalinda wakulima wadogo wa Taveta.
Katika hotuba yake, aliweka wazi kilio cha wakaazi na wakulima wadogo wa Taveta na aliweza kupeana hoja zake katika masuala yafuatayo;
(a) Tishio la wanyamapori lililoshuhudiwa katika sehemu nyingi za Taveta;
(b) Riba kubwa ya mikopo ya AFC kwa wakulima waliopata ardhi kupitia AFC;
(c) Kuchelewa kwa Serikali kurejesha Ardhi ya Machungwani kwa wakazi wa Taveta;
(d) Ushindani wa soko la ndani unaofanywa na Twiga Foods na wakulima wengine wakubwa;
(e) Ada za juu za Serikali ya Kaunti kwa ndizi, Nyanya, Vitunguu na mazao mengine ya shambani;
(f) Kukataliwa kwa maji katika shamba la Gicheha kwa wakazi wa Sir Ramson, Lumi, na Sehemu ya Njukini.
Mbunge huyo wa Taveta alieleza umuhimu na jukumu la Twiga Foods, KWS, AFC, na Serikali ya Kaunti kuhakikisha wamewalinda wakulima wadogo wa eneo hilo.
Matukio haya yamejiri baada ya kampuni ya Twiga kujingiza mzima mzima katika shughuli za ukulima tofauti na zamani ambapo wangenunua bidhaa kutoka kwa wakulima. Hatua hiyo ya Twiga ya kujiunga na ukulima eneo hilo limepokelea na maoni tofauti kutoka kwa wakaazi wa Taveta hasa wakulima, wengine wakilalama hatua hizo kwani zinahujumu wakulima wadogo na wala haziwanufaishi ikilinganishwa na zamani
Wakaazi wengine wanaunga hatua ya Twiga kujiunga na ukulima wakidai ya kuwa imesaidia kuajiri watu sehemu hiyo.
Kupitia ukurasa wa facebook wa mbunge huyo, Mkurugenzi mtendaji wa Twiga Foods ameonyesha nia ya kufanya mazungumzo na kuwashirikisha wadau wa Taveta na wakulima wote wadogo wa Nyanya na vitunguu ili kuona namna gani wanaweza kufaidika na Twiga Foods.
Ili kupata habari zetu kwa haraka jiunge na channel yetu ya Telegram kwa kuonyeza hapa