MAAFISA WA KIJASUSI WAWAKATAI VIJANA WA KUNDI LA UHALIFU MOMBASA.
Kufuatia operesheni inayoongozwa na maafisa wa kijasusi katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mombasa, wamefanikiwa kuwakamata watu watano wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la uhalifu ambalo limekuwa likiendesha shughuli zake katika eneo la Sargoi na vitongoji vyake.
“Kufuatia operesheni iliyoongozwa na kijasusi, timu ya maafisa walio katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mombasa wamewakamata watu watano wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la uhalifu lililopangwa ambalo limekuwa likiendesha shughuli zake katika eneo la Sargoi na vitongoji vyake,” taarifa ya DCI . .
Washukiwa hao watano ambao ni Vincent Ochieng, Shadrack Ochieng, Felix Otieno, Salim Ali na Shafi Yusuf awali walinaswa kwenye rekodi ya video huku wakionyesha vitu walivyoiba kutoka kwa waathiriwa wao.
Baada ya kunaswa, iphone tatu, simu ya samsung, simu ya memojo, headphone ya bluetooth miongoni mwa vitu vingine vilipatikana kutoka kwao. Watano hao wamezuiwa wakisubiri kufikishwa mahakamani.