Kalonzo Afanya Mazungumzo Ya Faragha Na Raisi Uhuru

Share this story

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka siku ya Ijumaa jioni alimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta nyumbani kwake Karen Nairobi amabapo walifanya mkutano wa faragha na mwenyekiti wa kanu Gideon Moi.

Mkutano huo unajiri kufuatia wasiwasi wa Kalonzo kuhusu mkataba wa Azimio La Umoja ambao ulitiwa saini wakati wa Kongamano la Wajumbe wa Kitaifa la Azimio lililoandaliwa mwezi uliopita katika jumba la KICC ambapo rais alimuidhinisha Raila kuwania urais.

Kalonzo alidai kuwa hakufahamu kilichokuwa ndani ya stakabadhi zilizotiwa saini ambazo ziliunganisha vyama katika muungano wa Azimio La Umoja.

Kalonzo alisema kuwa atamuunga mheshimiwa Raila Odinga mkono kuwania kiti cha Uraisi mwenzi wa Agosti ila alisisitiza mkataba alioweka saini kati yake na wenzake ni mkataba wa Azimio One Kenya Aliance na wala sio Azimio La Umoja kama wanavyodai wenzake

"Ilikuwa furaha na furaha yangu kabisa kuwakaribisha Rais wa Jamhuri ya Kenya H. E Uhuru Muigai Kenyatta na mwenzangu wa OKA Seneta wa Baringo.
 @MoiGideon
 katika makazi yangu ya Nairobi jana jioni" Aliandika katika tuvuti yake ya twitter


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post MP Washiali Warns Kenya Kwanza as Ruto Ally Confronts Malala Over Dp Post
Next post Agano Party Endorses Lawyer, David Waihiga Mwaure, As Its Presidential Flag-Bearer in the August 9 elections.