Israel yashambulia bandari ya Yemen baada ya waasi wa Houthi kushambulia Tel Aviv

Share this story

Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch limeripoti kwamba shambulio la Israel katika bandari muhimu ya Hodeida nchini Yemen litapelekea hali mbaya ya kibinadamu nchini humo kutokana na kwamba bandari hiyo ndio iliyokua ikitegemewa kama kitovu cha uchumi wa taifa hilo(taarifa hiyo nmekuekea hapo chini kwenye comments)

Baada ya waasi wa Houthis kushambulia ndani ya Israel kwa makombora, Israel ilijibu uchokozi huo kwa shambulio moja kubwa na baya lililoangamiza kabisa bandari hiyo muhimu nchini Yemen.

Hata hivyo toka Israel ipige shambulio hilo moja waasi wa Houthis wameishiwa nguvu na kupunguza kasi ya mashambulizi yao katika ukanda mzima

Israel walionya kwamba hilo ni onyo tu ila Houthis wakithubutu kushambulia Israel tena watapata majibu mabaya zaidi

Bandari hiyo inatajwa kuwa ilikua inategemewa kwa shughuli zote za kiuchumi nchini humo ikiwemo biashara ya mafuta, misaada ya kibinadamu, uingizaji wa bidhaa muhimu sambamba na silaha

Shirika hilo limeonya kwamba kuharibiwa kwa bandari hiyo kunaweza kusababisha njaa kwa mamilioni ya watu nchini humo


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post 8 Police Officers Interdicted After 13 Suspects Escape From Gigiri Police Station
Next post Israel yajibu mashambulizi bandari ya Yemen baada ya waasi wa Houthi kushambulia Tel Aviv