Hussein Mohammed atawania kiti cha urais cha FKF huku McDonald Mariga akiwa mgombea mwenza wake!
Kiungo wa kati wa zamani wa Inter Milan na Timu ya Taifa ya Kenya, McDonald Mariga, anatarajia kutangazwa rasmi leo Ijumaa kama mgombea mwenza wa Hussein Mohammed ambaye anawania Urais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF).
Uchaguzi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) umeratibiwa kufanyika tarehe Disemba 07, 2024.
McDonald Mariga Wanyama ameweka rekodi hizi:-
Mkenya wa kwanza kucheza LaLiga
Mkenya wa kwanza kucheza Serie A
Mkenya wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa barani Ulaya
Mkenya wa kwanza kushinda Ligi ya Mabingwa barani Ulaya