Harambee Stars Kucheza Mechi Zake Ugenini

Share this story

Timu ya Taifa ya Harambee Stars itacheza mechi zake nje ya Kenya kufuatia viwanja nchini humo kutokidhi vigezo vilivyowekwa na CAF.

Kenya inatarajia kucheza michezo miwili dhidi ya Burundi na mwingine na Ivory coast mwezi Juni katika ushindani wa kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Baada ya CAF kufanya ukaguzi imesema kuwa viwanja vya Nyayo na Ulinzi Stars havikidhi vigezo kwa ajili ya kupokea mechi za Kimataifa.

Kenya inaweza pia ikakumbana na shoka la FIFA kutokana na mgogoro uliopo ndani ya shirikisho baada ya serikali kutaka kuingilia masuala ya soka.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Thiago Silva set to leave Chelsea at the end of this season
Next post Mackenzie Abandons Him Fails To Appear In Court