Diamond Platnumz Asema Alilipwa Ksh 129 Milioni Kwa Kutumbuiza Kwenye Harusi Ya Mtoto wa Tajiri Maarufu Mjini Mombasa.
Jana imefanyika harusi ya mtoto wa mfanyabiashara mkubwa huko Kenya anayeitwa Imran Khosla. Walioalikwa ni watu maarufu tu, Diamond Platnumz pamoja na Nandy nao walialikwa. Kwenye Picha ni Rais Ruto pamoja na viongozi wengine wa Kenya. Kwenye comment ni video za magari yaliyoingia kwenye harusi.
Diamond Platinumz alifichua kuwa alilipwa Ksh128 milioni huku Nandy akifichua kuwa alilipwa Ksh45 milioni kwa onyesho la dakika 10 kwenye harusi ya mwana wa Imran Khosla.