AJALI YA WANAFUNZI WA KENYATTA: SERIKALI YA KAUNTI YA TAITATAVETA KUSIMAMIA GHARAMA ZA MATIBABU

Share this story

Serikali ya kaunti ya Taita Taveta imetangaza kusimamia gharama zote za matibabu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta waliohusika kwa ajali huko Maungu kwenye barabara kuu ya Nairobi kuelekea Mombasa.

Akizungumza baada ya kuwatembelea wanafunzi hao katika hospitali ya Rufaa ya Moi, Voi Gavana Andrew Mwadime-Wakujaa amepongeza juhudi za wahudumu ambao wanaendelea kuwauguza waliojeruhiwa.

Kulingana na ripoti ya hospitali, kati ya majeruhi 24, 18 wamefanikiwa kutibiwa na kuruhusiwa kujiunga na familia zao huku miili ya wanafunzi 11 ikihifadhiwa katika makafani ya hospitali hiyo hiyo.

Gavana Mwadime aidha amewataka madereva kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani ili kuepuka ajali.

Manusura kumi na mmoja wamesafiririshwa na ndege huku wengine wakitarajiwa kusafirishwa kutumia ambulansi kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi katika hospitali ya Parklands Avenue jijini Nairobi.

Ajali hii inajiri siku Moja baada ya nyingine kutokea eneo la Mariwenyi barabara kuu ya Voi-Mwatate ambapo mtu mmoja alidhibitishwa kufariki.

Imenukuliwa kupitia TaitaTaveta County Government


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Takehiro Tomiyasu Sign New Contact To 2026
Next post TAITATAVETA COUNTY SET HOST TREE PLANT EVENT AT KISHENYI DAM AS WORLD CELEBRATE TREE PLANTING DAY TOMORROW