Aliyekuwa gavana Samboja arudi kijijini kusema ‘asante’ kwa kura 5
Aliyekuwa Gavana wa Taita Taveta Granton Samboja amerejea wadi moja Taitataveta kusema asante kwa kura chache alizopata kwenye uchaguzi wa Agosti 9. Imebainika kuwa alipata kura tano katika wadi hiyo.
Gavana huyo wa zamani alisema amerejea katika wadi kuwashukuru kwa usaidizi wao, haijalishi ni mdogo kiasi gani.
“Nimerudi kijiji cha Mkamenyi, Wodi ya Kasigau kusema asante kwa kupigiwa kura tano katika uchaguzi uliopita. Uongozi hutoka kwa Mungu. Ninasema asante,” Samboja alisema.
“Vilevile, nimetoa mchango wangu kwa minajili ya kumsaidia Ngoa Kombo anayejiunga na chuo kikuu cha Nairobi” Aliongeza.