Mbabe wa dawa ya kulevya El Mayo akiri makosa yake

Share this story

Aliyekuwa mbabe wa genge la magendo nchini Mexico Ismael “El Mayo” Zambada amekiri mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Marekani. 
Zambada Aliomba radhi na kusema kuwa anabeba dhamana kikamilifu kwa matendo yake.

Alisema anasikitika kwa kusaidia kujaza nchini Marekani dawa za kulevya aina ya kokeini, heroini na dawa zingine haramu na kwa kuchochea ghasia mbaya nchini Mexico. Aliomba radhi na kusema kuwa anabeba dhamana kikamilifu kwa matendo yake.

Waendesha mashtaka wamesema chini ya uongozi wa Zambada na Joaquin “El Chapo” Guzman, kikundi cha Sinaloa kilibadilika kutoka ngazi ya kikanda hadi kuwa mtandao mkubwa zaidi wa biashara ya madawa ya kulevya duniani.

Zambada alikamatwa huko Texas mwaka jana, mwishoni mwa utawala wa Biden, wakati mfanyabiashara huyo wa madawa ya kulevya alipofika kwa ndege ya kibinafsi katika uwanja wa ndege wa Texas akiwa na mmoja wa watoto wa Guzman, Joaquín Guzmán López. 


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Ruto grants Harambee Stars Sh1 million each for affordable housing, increases athlete rewards
Next post Morocco Beat Madagascar to Win CHAN Cup