Cristiano Kuweka Rekodi Ya Mkataba Mpya Uraibuni

Share this story

Cristiano Ronaldo yuko mbioni kusaini mkataba mnono mpya ambao utamfanya kuwa mwanasoka anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani.

Al-Nassri inayoshiriki Saudi Pro League imetajwa kumpatia Cr7 mkataba wenye thamani ya zaidi ya pauni £167.9million (€200m) tofauti na Nyota wa Inter Miami, Lionel Messi anayeingiza takriban pauni milioni 103 kwa mwaka.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 alijiunga na klabu hiyo Januari 2023 baada ya kuondoka Manchester United, kwa sasa anaingiza takriban pauni milioni 164 kwa msimu kutokana na kiwango chake uwanjani, huku pauni milioni 49 za mshahara wake zikitoka katika shughuli za nje ya uwanja. mchanganuo wa malipo utamfanya apate £3.19m ( €3.8m) kwa wiki na £419,800 (€500,000) kwa siku.

Je, ni kazi gani nyingine inaweza kukulipa zaidi tofauti na mpira wa miguu?


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post CAF Postpones CHAN To August 2025
Next post Cristiano Ronaldo Anunua Private Jet Mpya Yenye Thamani ya Dola Milion 75