MARUFUKU YA KUUZA VYUMA CHAKAVU NCHINI KENYA
Rais Uhuru Kenyatta ametoa amri ya kusitishwa kuuzwa kwa vyuma chakavu nchini Kenya hadi mipango kamili itakapo wekwa. Raisi aliagiza kutozwa malipo ya uhaini kwa wakenya watakaopatikana na vyuma vya umeme.
Akizungumza mnamo Alhamisi, Januari 20, katika Kampasi Kuu ya Chuo cha Kitaifa cha Polisi, Kiganjo katika Kaunti ya Nyeri, Uhuru aliamuru polisi kutokuwa na huruma wanapokabiliana na wahalifu watakao patikana wakiuza vyuma chakavu. Rais pia alitangaza marufuku ununuzi na kuuza vyuma chakavu hadi pale serikali itakapoweka miongozo ifaayo ya kudhibiti viwanda na kudhibiti uhalifu.
Hii ni baada ya kukatika kwa umeme nchini Kenya uliotokea mnamo tarehe 11 january 2022.
Kulingana na uchunguzi unaonyesha nguzo hizo za njia ya umeme zilianguka kutokana na uharibifu na wizi wa vyuma vya nguzo hizo za umeme.