Afisa wa kaunti ya Taita Taveta akamatwa kwa madai ya ubadhirifu
Afisa mkuu wa kaunti ya Taita Taveta amekamatwa na maafisa wa upelelezi wa EACC. Duru za kuaminika zinasema mshukiwa huyo anasindikizwa hadi katika Afisi ya EACC Mkoa wa Mombasa kwa hatua zaidi.
Afisa huyo anakabiliwa na madai ya ubadhirifu wa zaidi ya milioni saba, ambayo yanahusisha MCAs 30 na maafisa wengine wakuu wa kaunti.
Inasemekana walitumia fedha hizo kwa safari ya Zanzibar ambapo baadhi ya waliolipwa hawakusafiri huku wengine wakilipwa zaidi.
Kukamatwa huko kunajiri baada ya shirika la kupambana na ufisadi kuchapisha Ripoti yake ya Robo ya Nne ya mwaka mnamo Ijumaa, ambapo faili mbili kati ya 24 zinazopendekeza kufunguliwa mashtaka kwa washukiwa zinahusiana na Taita Taveta.