TAITATAVETA : MAWAZIRI WATIA SAINI MKATABA WA UTENDAKAZI

Share this story

Mawaziri kutoka wizara zote Kaunti ya TaitaTaveta hii leo wametia Saini mkataba wa utendakazi,kwenye hafla ilioongozwa na Governor Andrew Mwadime – Wakujaa na naibu wake H.E. Christine Saru Kilalo

Akiongea wakati wa zoezi hilo Gavana Wakujaa amewataka mawaziri kuwajibika ipasavyo.

“Kile nahitaji kuona kutoka kwenu ni uwajibikaji kwenye majukumu niliyowapa.Naamini mna uwezo,nataka kuona kazi zikitekelezwa vilivyo kwani mwananchi anachoangalia kwa sasa ni huduma.Yeyote ambaye hatowajibika hana nafasi kwa serikali yangu.”amesema.

Mkataba huu utakuwa ukifanyiwa tathmini Kila baada ya Miezi mitatu.

Naibu Gavana Bi Christine Kilalo kwa upande wake amewataka mawaziri ambao ndio kiungo kikuu katika utekelezaji wa agenda ya gavana kuhakikisha ,wanafahamu fika agenda na malengo ya Uongozi wa Wakujaa.

“Nyinyi ndio nguzo, mfahamu Gavana Wakujaa aliwaamini na kuwapa nafasi mnazoshikilia kwa Sasa, wakati ni Sasa mthibitishe hilo kwa kuhakikisha mnachapa kazi kwa lengo la kuafikia ndoto ya maendeleo kama ilivyo kwa Manifesto yetu.”

Mawaziri waliotia Saini mkataba huo aidha wametoa hakikisho kuwa watawajibika kwenye sekta zao,kwa uaminifu.

Via The TaitaTaveta County Government


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Willis Raburu Lands New Role At TV47 As Director of Digital Services
KBC's acting Managing Director Samuel Maina. | PHOTO: @SamCMaina/X Next post CS Owalo Fires KBC Managing Director Over Ksh770billion Fraud