Wavumbuzi wa miundo ya kiuchumi ya “Bottom UP” wakutana hatimaye

Share this story

Rais William Samoei Ruto hatimaye alipatana na Raisi wa Marekani Joe Biden, kwenye tafrija iliyoandaliwa na Biden wakati wa Kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York.

Viongozi hao wawili wanapigia debe mfumo wa uchumi wa “Bottom UP” wenye umeleta msisimuko kwa wengi ukimwezesha Raisi William Ruto kushinda uchaguzi wa uraisi nchini Kenya.

Kulingana na maraisi hao wawili wamekuwa wakipigia debe mfumo huo wakisema kwamba mfumo wa uchumi wenye umekuwa ukitumika wa “Trickle Down” hajafaidi wanaichi na ni wakati wa kujenga uchumi wa nchi kuanzia chini kwenda juu.

Rais wa Marekani Joe Biden alielezea nia yake ya kufanya kazi kwa karibu na Rais wa Kenya William Ruto ili kufikia mustakabali mzuri zaidi na salama kwa Wakenya na kwa ushirikiano thabiti kati ya Marekani na Kenya.

Raisi William Ruto aliandamana na mkewe Rachael Ruto kwenye hafla hiyo


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Mshtakiwa achapa usingizi wa pono na kukoroma hakimu akimsomea mashtaka
Next post Azimio wants Chebukati reinstate Ruth Kulundu