Trump, Ametunukiwa Tuzo La Amani La FIFA

Share this story

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametunukiwa Tuzo la Amani la FIFA kwenye hafla ya sare ya hatua ya makundi ya kombe la Dunia 2026, iliyofanyika leo Ijumaa, Desemba 5, 2025, huko Kennedy Center, Washington, D.C.

FIFA imesema tuzo hiyo, inayojulikana kama “FIFA Peace Prize – Football Unites the World”, inalenga kutambua watu waliofanya matendo ya kipekee ya kuleta amani na kuwaleta watu pamoja kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Hata hivyo, vigezo vya uteuzi na mchakato wa kuchagua washindi bado haujawekwa wazi, jambo ambalo limeibua maswali kutoka kwa wadadisi wa masuala ya haki na uwazi.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Neymar Afunga Hat-Trick Kuokoa Klabu iliyomlea!
Next post MP calls for tax and levy exemptions for the disabled