Tajiri Elon Musk Kupitia Kampuni Yake Ya Tesla Azindua Robotaxi & Robovan

Share this story

Mmiliki wa Kampuni ya TESLA ambaye pia ndioTajiri namba moja duniani kwa sasa, Elon Musk, leo huko California Marekani, amezindua Basi jipya na la kisasa liitwalo ROBOVAN ambalo lina uwezo wa kubeba Abiria 20 na kujiendesha bila Dereva.

Inaripotiwa kuwa Basi hilo la ROBOVAN ambalo linatarajiwa kuingia sokoni kabla ya mwaka 2027, linatumia teknolojia ya camera na akili bandia bila ya kuwa na vifaa muhimu vya uendeshaji kama vile usukani au kanyagio katika magari mengine ambapo licha ya kuuzwa, Watu mbalimbali watakuwa na uwezo wa kulikodi kupitia APP maalum ya TESLA kwenye simu zao.

Haya yatakuwa mapinduzi ya aina yake ndani ya Kampuni ya TESLA kwani yatakuwa ni sehemu ya magari yake mapya yasiyo na usukani wala kanyagio tofauti na TESLA za sasa ambazo zinazo.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Court of Appeal Overturns High Court Decision to Convict MP Waluke to 67 Years in Prison
Next post FT: Cameroon 4-1 Kenya