Spika wa Baraza La Wawakilishi La Marekani Atimuliwa
Kevin McCarthy ametimuliwa kama spika wa Baraza la Wawakilishi katika uasi wa kikatili na wa kihistoria wa Warepublican wa siasa kali za mrengo wa kulia waliokasirishwa na ushirikiano wake na upande wa Democrat.
Tukio hilo linafichua viwango vya ndani vya machafuko kati ya Warepublican wanaoelekea kwenye uchaguzi wa urais wa 2024, na bila shaka ukioongozwa na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ambaye anaweka historia yake kama rais wa kwanza wa zamani anaelengwa kuwa na mashtaka mengi ya jinai.
Wabunge 8 wa chama cha Republican walipiga kura kwa kushirikiana na wabunge wote wa upande wa chama cha Demokrat kumwondoa McCarthy, ambaye kwa sasa anasalia kuwa mbunge wa kawaida baada ya kuondoka katika kiti cha uspika.