RASMI IBRAAH AMEMALIZANA NA KONDEGANG

Share this story

Rasmi sasa Chinga @ibraah_tz amemalizana na lebo aliyokuwa akifanya nayo kazi Konde Music Worldwide baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati yake,lebo hiyo na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
Makubaliano hayo yamesainiwa mbele ya Katibu Mtendaji wa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana, Ibraah aliambatana na mshauri wake wa biashara, Bw. Msigwa na upande wa Konde Gang ukiwakilishwa na wakili wao, Bi. Sandra.


Kupitia makubaliano hayo, Ibraah ameruhusiwa kuendelea na kazi zake za muziki bila masharti yoyote kutoka kwa lebo hiyo. Hatua hii inatoa nafasi kwa msanii huyo kujiendeleza zaidi kisanaa kwa uhuru na ubunifu wake binafsi.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Fukwe Zote za Umma Mombasa Zimefungwa