Rais William Ruto amuongeza Waziri Mkuu Musalia Mudavadi majukumu zaidi katika mabadiliko ya baraza la mawaziri
Rais William Ruto amefanya mabadiliko ya Makatibu Wakuu wanane kwa wizara mbalimbali katika mabadiliko ya hivi punde ya baraza la mawaziri yaliyolenga kulainisha utendakazi huku Mkuu wa Nchi akitarajia kutimiza ahadi zake za uchaguzi.
Katika mabadiliko hayo Raisi amemuongeza Waziri Mkuu, Musalia Mudavadi, majukumu zaidi ikiwepo kumfanya Waziri wa Mambo ya Nje.
Musalia katika taarifa aliyoitoa kufuatia mabadiliko hayo alitangaza kuwa yuko tayari kushughulikia majukumu aliyoongezwa.
“Nimefurahishwa sana kwa kukabidhiwa na Mheshimiwa Rais William Samoei Ruto jukumu kubwa katika Baraza la Mawaziri lililofanyiwa mabadiliko,” sehemu ya taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ilisoma.
“Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa kwa imani aliyoniwekea kwa kunikabidhi jukumu muhimu zaidi la Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora.” Mudavadi alifichua kuwa atatekeleza jukumu lake la kulinda maslahi ya Wakenya, ndani ya mipaka yetu na nje ya nchi.