Polisi Wawakamata Waandamanaji wa Mombasa Huku Maandamano ya Kupinga Utekaji nyara Yakiendelea
Polisi wameripotiwa kuwakamata waandamanaji kadhaa waliojiunga na maandamano ya kupinga utekaji nyara mjini Mombasa nchini Kenya.
Huku maandamano yakianza katika maeneo kadhaa ya nchi baada ya kampeni ya mtandaoni dhidi ya serikali, polisi wa kupambana na ghasia walikuwa wamejiandaa ili kuweza kuzima uwezekano wa moto wa maandamano hayo.