Mtangazaji wa kituo cha Wasafi FM kupitia kipindi cha “Mashamsham”, Dida Shaibu afariki Dunia.
Mtangazaji wa Wasafi FM kupitia kipindi cha ‘Mashamsham’, Khadija Shaibu maarufu kama Dida alifariki Dunia usikuwa Ijumaa, Oktoba 4, 2024 baada ya kuugua na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa za msiba huo zilithibitishwa na mtangazaji mwenzake, Maulid Baraka Kitenge kupitia mitandao yake ya kijamii.
Kitenge aliandika; “Dida shaibu wa Wasafi FM amefariki dunia.”
Didah alifikwa na umauti akiwa na umri wa miaka 42, ambapo kifo chake kimetokea siku kumi na sita (16) toka Wafuasi wake washuhudie ukimya wake katika mitandao ya kijamii ambapo chapisho lake la mwisho mtandaoni lilikuwa Septemba 19, 2024 ambapo aliweka picha yake akiwa kwenye gari ikisindikizwa na wimbo wa Martha Mwaipaja “Amenitengeneza”.
Kabla ya kutua Wasafi, Dida alikuwa akifanya kazi ya utangazaji katika kituo cha Times FM kupitia kipindi cha Mirindimo.