Mshtakiwa achapa usingizi wa pono na kukoroma hakimu akimsomea mashtaka

Share this story

Mapya yaibuka! Mdada mmoja mjini Nairobi kwa jina la Sharon Oparanya amedakwa akiendesha gari aina ya Mercedes Benz akiwa amelewa mida ya asubuhi hivyo kushindwa hata kudhibiti uendesheji wake katika barabara ya umma.

Kana kwamba hiyo haitoshi, baada ya kuburutwa mahakamani hapo hapo mahakamani akauchapa usingizi wa pono na kuanza kukoroma mtindo mmoja ambapo mkoromo wa hali ya juu aliokuwa akiutoa ulimshtua hadi hakimu na kuwaacha watu midomo wazi mahakamani hapo

Hivyo, hakimu kuamuru akatupwe rumande kwanza hadi ijumaa hii ndio apande tena kizimbani kujibu mashitaka

Alikamatwa tarehe 22 september hii


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Babu Owino Accuses ODM Leadership of Betrayal
Next post Wavumbuzi wa miundo ya kiuchumi ya “Bottom UP” wakutana hatimaye