Mbosso amuhenzi mwalimu wa shule ya msingi aliyeubadilisha wimbo wake wa ‘Pawa’
MSANII Mbwana Yusuf Kilungi, maarufu Mbosso, amemshangaza mwalimu wa shule ya msingi baada ya kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 388 hadi Tanga Hills, ambako ndiko anakoishi mwalimu huyo, kwa ajili ya kumuenzi kwa zawadi za gharama kubwa kutokana na kubadilisha wimbo wake wa Pawa.
Mwalimu alikuwa ametengeneza upya maandishi ya wimbo huo maarufu kwa ubunifu, na kuyarekebisha kuwa sehemu ya kuwatia moyo wanafunzi wake.