Mamlaka nchini Marekani Imetangaza kumkamata kijana aliyemuua mwanaharakati maarufu wa maadili nchini humo Charlie Kirk

Share this story

Mamlaka nchini Marekani imetangaza kumkamata kijana aliyemuua kwa risasi mhubiri na mwanaharakati maarufu wa maadili nchini humo Charlie Kirk siku ya juzi

Taarifa iliyotolewa na vyombo vya usalama imeeleza kwamba kijana huyo Tyler Robinson baada ya kufanya mauaji hayo alirudi nyumbani na kumsimulia baba yake mzazi ambaye alimuweka chini ya ulinzi na kuwaita polisi kuja kumkamata

Baba yake mzazi ni mwanajeshi mstaafu wa jeshi la Marekani aliyefanya kazi jeshini zaidi ya miaka 27 na hata mafunzo ya matumizi ya silaha kijana huyo alipata kwa baba yake ikiwemo umahiri wa kulenga shabaha (ulengaji/usniper)

Tyler kijana wa miaka 22 alikua mwanafunzi katika chuo cha Utah ambapo Charlie Kirk alikuwa na mhadhara na ndipo Tyler alipotumia nafasi hiyo kwenda kutekeleza mauaji hayo kwa kumlenga risasi kutokea juu ya jengo refu

Unadhani ni kwann vijana wengi wa kishua mara nyingi wanakuwa vijana wa ovyo na wengi wanafanya mambo ya ovyo?


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Charlie Kirk Aaga Dunia
Next post Interior PS Omollo inspects Ithookwe Stadium ahead of Mashujaa Day celebrations