FIFA : Unaweza kufungwa jela miaka 7 iwapo utapatikana ukifanya ngono nje ya ndoa wakati wa kombe la dunia, nchini Qatar
FIFA imetoa onyo ya kuwa mbinu kali zitatumika kuzuia vitendo vya kufanya mapenzi nje ya ndoa katika mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Qatar.
Vitendo vyote vya kufanya mapenzi kati ya watu ambao si wanandoa havitovumilika.
“Ufanyaji mapenzi kiholela umepigwa marufuku kwenye Kombe la Dunia la mwaka huu. Mashabiki mnaombwa kujiandaa. Kila mmoja atatakiwa kujilinda mwenyewe.”
Nchini Qatar ufanyaji wa mapenzi nje ya ndoa hukumu yake ni kifungo cha jela kinachoweza kufikia miaka 7.
Nchi ya kiarabu ya Qatar ina sheria kali ambayo inakataza kufanya mapenzi nje ya ndoa nchini humo. Wakati raia wa Qatar tayari wamezoea sheria na kanuni, wale wanaosafiri kwenda nchini humo kutazama Kombe la Dunia watalazimika kuhakikisha wanafahamu sheria za nchi.
Kwa mujibu wa sheria, hakuna mtu anayeweza kufanya mapenzi nje ya ndoa nchini Qatar na wale wanaopatikana na hatia wanaweza kufungwa jela zaidi ya mwaka mmoja, kulingana na ripoti. Hata hivyo, kulingana na shirika lisilo la faida la Human Dignity Trust, walio na hatia wanaweza pia kufungwa jela miaka saba iwapo watapatikana wakikiuka sheria katika taifa.
Mashabiki wanakumbushwa kwamba japokuwa pombe si kinyume na sheria nchini humo, hairuhusiwi kabisa kunywa hadharani na pia kulewa hadharani ni kosa.
Kingine ni kuwa yoyote atakayekutwa akitumia dawa za kulevya aina ya cocaine hukumu yake ni kifo.