DOGO JANJA ATUHUMIWA KUMPIGA MWANAFUNZI RISASI .
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema linafanya uchunguzi wa tukio la Bakari Halifa Daud (18), mkazi wa Sombetini Jijini Arusha kujeruhiwa kwa risasi mguuni na Mgombea Udiwani Kata ya Ngarenaro (CCM), Abdulaziz Abubakari Chande (30), maarufu Dogo Janja.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 23, 2025 saa 5:30 usiku huko katika maeneo ya Sombetini.
Kamanda Masejo amesema mgombea huyo ambaye ni mkazi wa Levolosi amedai wakati akiwa anashuka kwenye gari alitaka kuvamiwa na Bakari Halifa akiwa na mwenzake kwa kutumia silaha ya jadi, hali iliyopelekea kutumia silaha aliyokuwa nayo kwa nia ya kujihami.