Charlie Kirk Aaga Dunia

Share this story

Marekani na dunia ilimpoteza kijana shujaa wa maadili mema Charlie Kirk ambaye alipigwa risasi na watu ambao bado hawajafahamika katika mkutano huko chuoni Utah nchini Marekani

Charlie amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuongoza kampeni dhidi ya tabia za upinde na ibada za kishetani ambapo amekuwa akiongoza mijadala mikubwa na kupinga vikali mambo hayo ambayo amekuwa akiyataja kama mambo maovu mno kwenye jamii.

Charlie alikuwa mshirika mkubwa wa rais Trump kipindi cha kampeni akimuunga mkono kwa misimamo yake ya kupinga upapai na kurudisha maadili ya nchi kwenye misingi sahihi

Tayari vyombo vya usalama vimeshamkamata mtuhumiwa mmoja aliyekuwa eneo la tukio risasi ilipopigwa kutoka jengo refu, rais wa Marekani Donald Trump amelaani mauaji ya Charlie na kusema hakuna aliyehusika atakayesalimika mbele ya sheria

Charlie kijana mzaliwa wa 1993 tayari alikuwa mwanaharakati mkubwa anayeaminika na kutetea maadili mema kwenye jamii Marekani na duniani kote


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Harambee Stars thrash Seychelles 5-0 in dominant World Cup qualifier win
Next post Mamlaka nchini Marekani Imetangaza kumkamata kijana aliyemuua mwanaharakati maarufu wa maadili nchini humo Charlie Kirk