Charity Kaluki Ngilu ajiondoa kwa kinyang’anyiro cha ugavana katika kaunti ya Kitui

Share this story

Gavana wa Kitui Charity Ngilu hatatetea kiti chake katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Agosti 9.

Uamuzi wa Ngilu kujiondoa katika kinyang’anyiro cha ugavana uliwekwa wazi na mgombeaji urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga wakati wa ziara yake katika kaunti ya Kitui mnamo Jumatano, Juni 15.

Akitoa tangazo hilo, Raila alibainisha kuwa Ngilu badala yake angeelekeza nguvu zake katika azma yake ya urais wa kitaifa na kuahidi kumteua iwapo ataunda serikali ijayo.

“Mtaamua kati ya aliyekuwa gavana Julius Malombe na aliyekuwa seneta David Musila ambaye atakuwa gavana wenu. Ninataka kumpeleka mama Nairobi,” Raila alisema.

“Tuna Jubilee, ODM, Narc, Narc Kenya katika timu ya vyama 26… Ni nyinyi kuamua ni nani wa kumpigia kura miongoni mwa vyama kwani sote tuko Azimio,” alisema.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post MWANDISHI ALIYEANDIKA KITABU CHA JINSI YA KUMUUA MUME, AKUTWA NA HATIA YA MAUAJI YA MMEWE NA KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA.
Next post Raila’s Degree Surfaces, Raises More Questions