Chadema yatangaza siku saba za maombolezo
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kutokana na matukio ya kusikitisha yaliyosababisha vifo, majeruhi na kupotea kwa baadhi ya Wananchi siku ya October 29, Chama hicho kimetangaza rasmi siku saba za maombolezo.
Chama hicho kimeyaita maombolezo hayo kuwa ya kitaifa kuanzia leo November 05 mpaka November 11, 2025.
Akitangaza uamuzi huo jana November 04, 2025, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA Taifa, Brenda Rupia amesema ili kuonesha heshima kwa waliopoteza maisha, na kwamba bendera zote za CHADEMA katika ofisi za Chama zitapepea nusu mlingoti kila siku kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika siku zote saba za maombolezo.
Bado serikali haijatoa idadi ya watu waliopoteza maisha katika vurugu hizo zilizotokea Oktoba 29, ambapo ilikuwa siku ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.
