Azimio Haitatoa Notisi Za Maandamano Kwa Polisi Tena Asema Sifuna

Share this story

Senator wa Nairobi na ambaye pia ni mwanachama wa ODM Edwin Sifuna amesema kwamba chama cha upinzani cha Azimio hakitatoa tena notisi za maandamano kwa polisi kama inavyotakiwa na Katiba ya Kenya. Badala yake watatekeleza haki zao kupitia kifungu ch 37 cha katiba kichacho toa haki ya kuandamana kwa wakenya.

“Hatutatoa tena notisi. Hebu tutekeleze haki zetu chini ya Kifungu cha 37. Maandamano yatatokea yenyewe mahali popote, wakati wowote bila taarifa ya polisi kwa sababu tumegundua taarifa hizo ni mialiko ya wao kututumia vurugu,” aliambia Citizen TV.

Ingawa Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome awali aliambia mrengo unaoongozwa na Raila Odinga kutoa notisi kabla ya maandmano yaliyopangwa, muungano huo umesema hautatoa notisi tena kwa sababu ni haki yao.

Sifuna amedai polisi wamekuwa wakivuruga maandamano hayo kwa vurugu badala ya kutoa ulinzi kwa waandamanaji.

Azimio wamekuwa wakiandamana siku za Jumatatu na Alhamisi kupinga kile kinachodai utawala wa Rais William Ruto kushindwa kupunguza gharama ya maisha na upendeleo katika uteuzi wa Serikali, miongoni mwa masuala mengine.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post 14 confirmed dead so far after a Pwani University Bus collides with a 12 seater matatu in Naivasha Kayole Area towards Eldoret.
Next post DCI Arrests 14 Suspects After Jamia Supermarket Was Raided